Vurugu Za Zanzibar; Taarifa Za Hivi Karibuni...


Jeshi la Polisi Zanzibar limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha Uamsho waliokuwa wamekusanyika kufanya Dua ya kuwaombea watu waliokufa katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Skagit katika Mitaa ya Mbuyuni.
Habari kutoka Zanzibar zinadai kuwa Jeshi hilo la Polisi lililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kutokana na kikundi hicho cha Uamsho kuanza kuhubiri siasa badala ya kufanya Dua hatua iliyosabaisha kuvunjika kwa amani katika mitaa hiyo.

Mwandishi wa Kituo hiki cha Uhuru FM aliyeko Mjini Zanzibar amesema licha ya Watanzania kuendelea kuomboleza vifo vya watu waliokufa katika ajali hiyo, bado kikundi hicho cha Uamusho kimeendelea kufanya sisasa badala ya kufanya Dua.

Pia imeelezwa kuwa chanzo cha Mabomu hayo ya Machozi ni kikundi hicho kufanya Dua yenye utata huku masuala ya siasa yakijitokeza hatua iliyopelekea kuwepo kwa vurugu za hapa na pale hivyo Jeshi likaamua kutumia nguvu ya ziada ili kuwatawanya. 

CHANZO:  Radio  Uhuru FM