Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akifafanua jambo kwa
Naibu Waziri wa Uchukuzi (aliyavaa suti ya mikono mifupi), Dkt.
Charles Tizeba (Mb), wakati wa ziara ya siku moja katika Bandari ya Dar
es Salaam leo, kulia kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi ni Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Bw. John Mngodo, aliyevaa kofia nyeupe ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya kupakua na kupakia Makontena (TICTS), Bw.
Neville Bisett na Aliyevaa kizibao cha Kijani ni Meneja Msaidizi wa
Bandari ya Dar es Salaam,Bi. Winnie Mulindwa.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba akifafanua jambo kwa
uongozi wa Wizara, Bandari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha
Kupakia na kupakua makontena TICTS, kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Naibu
Waziri ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi Winnie
Mulindwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo(aliyevaa tai ya blue), Mhandisi
Omar Chambo, na Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Kupakua na Kupakia Makontena (TICTS), Bw. Neville Bisett.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Charles Tizeba (Mb),akiongea na baadhi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(hawapo pichani),wakati
alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam,Kushoto kwa Naibu
Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo,
Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo (wa pili kushoto),Bw. John Mngodo. Na
aliyevaa Kizibao ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam,Bi.
Winnie Mulindwa.
Meneja
Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Winnie Mulindwa, akitoa
taarifa ya namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (aliyeshika kichwa), ambaye
amefanya ziara ya siku moja katika Bandari ya Dar es salaam. Kushoto
kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo,
Kulia kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Bw. John
Mngodo, Kushoto kwa Meneja Bandari Msaidizi ni Mkurugenzi wa Idara ya
Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi,Bi. Tumpe Mwaijande.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya kupakua na kupakia makontena Bandarini (TICTS),
Bw. Neville Bisett akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.
Charles Tizeba (Mwenye Suti ya Mikono Mifupi),wakati alipofanya ziara
ya siku moja kuangalia ufanisi wa Kampuni hiyo katika Bandari ya Dar es
Salaam leo.Kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi,Bw. John Mngodo.Picha Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Uchukuzi