JOSE CHAMELEONE AFANYA MADUDU TENA....

Hivi karibuni msanii wa Uganda Jose Chameleone ameshindwa kuperform kwenye show ya nchini Norway baada ya kukosa visa ya kuingia nchini humo.
Tukio hilo limemfanya promoter aliyeandaa show hiyo ale hasara na kumuita Chameleone ni mwizi.

Baada ya promoter huyo kumuita hitmaker wa Valu Valu mwizi, jana ameutumia ukurasa wake wa Facebook kumjibu promoter huyo ambaye naye amemuita mbabaishaji baada ya kushindwa kumtafutia visa.



“I hate promotaz who blame artistes for their amateurism!! The Norway one is one of them he goes ahead organises a show and fails to get me a visa, what does he do? He calls me a thief upon his own failure.You can’t use amateur skills proffessionally!Get a life!”

July mwaka huu msanii huyo aliingia kwenye mgogoro mkubwa na Mkurugenzi wa Global Publishers Erick Shigongo aliyemtuhumu kumtapeli fedha hali iliyopelekea passport yake kushikiliwa na kumfanya aandamane hadi ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kuidai.