MAMA RAY C AKANUSHA UVUMI ULISAMBAA KUWA RAY C AMEFARIKI......


Usiku wa novemba 27 2012  zilisambaa  habari  za   msanii  Ray  c  zikidai  kuwa  amefariki  dunia.....


Habari  hizi  ziliwagusa  wengi  ambao  walitaka  kujua  undani  na  ukweli  wa  habari  hizo.Ukweli  ni  kwamba, Ray  c  ni  mzima  na  anaendelea  vizuri  na  matibabu


Mama  Ray  c  ameamua  kuvunja  ukimya  na  kuueleza  umma  kuwa  mwanae  ni  mzima.Wanaosambaza  habari  hizo  ni  adui  zake  tu.....


 “inasikitisha sana kusikia taarifa hizo, Ray C ni mzima kabisa namshukuru Mungu anaendelea vizuri na matibabu tuko nae, anakula vizuri anapata usingizi vizuri, hizo habari zimetoka wapi? nazikanusha kabisa kwa jina la Yesu nalikataa hilo neno” MAMA  RAY  C

Hivi  karibuni, hali  ya  Msanii  Ray  c  ilibadilika  na  kuwa  tete  kutokana  na  matumizi  ya  madawa  ya  kulevya  hali  iliyomfanya  mama  yake  aombe  msaada  kwa  wasamalia  wema  ili  kugharamia  matibabu  yake 

Haya  ni  mazungumzo   kati  ya mama Ray c na   milardayo   ambaye  ni  mtangazaji  wa  clouds  fm