RAIS KIKWETE AMTUNUKU BI KIDUDE NISHANI YA SANAA NA MICHEZO

Katika kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Tanzania jana Rais Jakaya Kikwete alimtunuku Nishani ya Sanaa na Michezo muimbaji mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Bibi Fatma Binti Baraka Khamis (Bi. Kidude) kwa mchango wa kipekee kwa taifa la Tanzania katika nyanja ya sanaa.Pamoja na Bi. Kidude, watu wengine katika makundi mbalimbali walitunikiwa nishani za heshima katika halfa iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.