MWANAMUZIKI wa Bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ametoa kali ya mwaka kwa kusema mademu wanamtongoza sana, jambo ambalo limekuwa kero kwake. Banza anadai kuwa kwa muda mrefu sasa hajawahi kutongoza mwanamke kwa vile wao ndiyo humtongoza.
Aidha, alisema idadi ya wanawake wanaomfuata wakimtaka kimapenzi ni kubwa ambapo wengi wao huwakataa na baadhi yao huwakubali kwa kuangalia maslahi anayoyapata kutoka kwao.
“Siku hizi dunia imebadilika sana, yaani nimeshasahau hata jinsi ya kutongoza,” alisema Banza.