MUME mtarajiwa wa staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka, Malick Bandawe
ameweka ‘plain’ kuwa licha ya kuwepo na utata wa hapa na pale, ndoa
yake na mwigizaji huyo bado iko palepale.Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni katika ofisi zao za Ndauka
Entertainment zilizopo Kinondoni jijini, Dar, Malick, alisema ndoa hiyo
itafungwa mwezi Novemba mwaka huu.
“Ndoa ipo palepale, kila kitu kitakuwa sawa Novemba mwaka huu. Familia zote mbili zimeshabariki ndoa hii kilichobaki ni maandalizi tu,” alisema Malick.