Poster ya Nataka kulewa Video.
Ile music video ya msanii Diamond Platnumz, ambao wimbo wake ulileta
utata baina ya wasanii watatu, namaanisha H-Baba, Pasha na yeye Diamond,
“Nataka kulewa” imekamilika na kilichobaki ni kuachiwa siku ya Jumapili
ya wikiendi hii.Kwa mujibu msanii Diamond na wa meneja wa msanii huyo Raqey ambaye
ndiye alikuwa muongozaji mkuu wa utayarishaji wa video hiyo, kila kitu
kimeshakamilika ikiwemo post production editing na sasa kilichobaki ni
kuachiwa rasmi siku ya Jumapili katika Street Bash Party iliyoandaliwa
na Clouds media kusherehekea kutimiza miaka 13 kwa kituo cha Radio ya
Clouds FM.