WAZIRI
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa leo ametangaza
matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2012 uliofanyika nchini kote
tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.
Katika
Mtihani huo Jumla ya wanafunzi 894,881 walisajiliwa kufanya mtihani huo
ambapo wavulana ni 426,285 sawa na asilimia 47.64 na wasichana ni
468,596 sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya wanafunzi hao, wapo
wanafunzi 874,379 ambao walitarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya
Kiswahili na wanafunzi 20,502 walitarajiwa kufanya kwa lugha ya
Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.
Wanafunzi
wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na
wasichana 39. Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi
makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.
Mtandao huu utawaletea habari kamili na link ya kupata matokeo hayo wakati wowote kuanzia sasa.