MITEGO YA KIMAPENZI YA AUNT LULU ILIGONGA UKUTA KWA KOFFI OLOMIDE


MTANGAZAJI mwenye matukio ya kumwaga Bongo, Lulu Mathias ‘Aunt Lulu’ alinaswa akihangaika kumtega mwanamuziki kutoka Kongo, Koffi ili aingie mkenge. Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar wakati mwanamuziki huyo alipokuwa akifanya shoo yake.
“Lengo la Aunt Lulu aliyevaa vazi lililomuacha mgongo wake kujipitishapitisha back stage alipokuwa amekaa Koffi lilikuwa kumnasa msanii huyo lakini hadi anapanda jukwaani hakufanikiwa hata kuongea naye,” alisema mdau aliyemshuhudia.
Alipoulizwa kuhusu ishu hiyo , Aunt Lulu alifunguka:

“Wewe chezea mimi, mwenyewe alidata na mapigo yangu, sema ndiyo hivyo alikuwa bize na shoo, najuta kumkosa” alisema Aunt Lulu .