KUFUATIA MAANDAMANO YALIYOFANYWA LEO NA CHUO KIKUU CHA ST. JOHN DODOMA ; MENGI YAIBUKA ...

 Maaskari wakiongoza msafara wa wanachuo ambao walikuwa wanaelekea kwa mkuu wa mkoa
 
 Maaskari wakiwa kwenye ulinzi wakati wa maanadamano ya wanachuo waliokuwa wanaelekekea kwa mkuu wa mkoa Dodoma
Uvumilivu sasa umetushinda!!! Hizi  ni kauli za wanafunzi wengi wa chuo Kikuu cha St.John walivyosikika wakizungumza kufuatia  kile ambacho kimeendelea kuvikumba baadhi ya vyuo  hapa nchini.  

Usiku wa kuamkia leo baadhi ya wanachuo  walivamiwa chumbani  na baadhi ya watu  wasiofahamika ambao walikata nondo za dirisha na kuiba Laptop tatu na simu tano na baada ya kuchukua vitu hivyo waliacha wamewafanyia vitendo vibaya na pia wanafunzi hao  waliachwa wamefungwa ili wasipige kelele.
Hali imepelekea  hisia kali za wanafunzi wa chuo hicho na kuamua kufanya maandamano kupinga vitendo hivyo  ambavyo  ni kinyume na haki za kibinadamu  na kusababisha  hali ya wanafunzi hao kusoma kwa mashaka  kutokana na mwendelezo wa matukio hayo.
Wanafunzi hao waliandamana leo kuelekea  katika ofisi za mkuu wa mkoa, kwa madai ya kutaka kukutana na mkuu huyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya mkoa  pamoja na kuhitaji kukutana na RPC kama  katibu wa kamati ya ulinzi ya mkoa ili wafikishe vilio zaidi.  
Hata hivyo  walisimama na kukaa kwa muda katika viwanja vya Nyerere square walipokuwa wakimsubiri mkuu wa mkoa. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari  mkuu huyo wa mkoa  hakuweza kuja katika viwanja hivyo, hatua iliyowalazimu wanafunzi hao kurudi chuoni.


 Wanachuo wakiwa wameshika mabango ya kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John



 Wanachuo wa chuo kikuu wakiwa kwenye maandamano
 Maaskari wakiwa nyuma ya maanadamano ya wanachuo wa chuo kikuu cha St. John
Wanachuo wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa hii ni kushinikiza ulinzi kwa sababu ya matukio ambayo yanaendelea kutokea maana juzi alifariki mwanachuo.