MHARIRI WA GAZETI LA BUSINESS TIMES APIGWA RISASI


Mnaku Mbani Lukanga (Mhariri wa gazeti la Business Times ) akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi alipohamishwa kutoka hospitali ya Temeke alikolazwa jana mara baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi hapo jana usiku katika mtaa wa Lugoda akiwa anaelekea nyumbani kwake Mbagala usiku wa saa mbili jioni.Katika tukio hilo, alikuwa na abiria wenzake 6 ambao nao walipigwa risasi.

Baadhi yao walitolewa risasi na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Mnaku alipigwa risasi juu yo mdomo na risasi hiyo kutokea kwenye shavu lake la kushoto. Bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari.