Vituko
mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja
kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16
mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na
hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.
Tukio lilikuwa hivi:
Zawadi kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi
hicho dada mtu huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake
ndipo mama yake mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi
mtaa wa mshindo.
Baada ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye
aliitika na kuingia ndani na ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi
alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa mama yake mdogo.
Katika kipigo hicho Zawadi alipigwa pamoja na
kunyweshwa mkojo kutoka kwa mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto
wa kuzaliwa na Dada yake Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na
tuhuma kwamba eti familia hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.
Zawadi inadaiwa aliwahi kwenda zanzibar kwa nia ya kufanya kazi na
baada ya muda mama yake mzazi ambaye jina lake bado halijafahamika
alimpigia simu arudi nyumbani na mara baada ya kurudi ndipo
kutokuelewana huko kukajitokeza.
Aidha taarifa za ndani kuhusu tukio hilo zinasema kuwa Mama yake
Msichana Zawadi alitupwa akiwa mchanga na kuokotwa na wasamalia wema na
hatimaye kulelewa na Bibi yake ambaye hata hivyo amefariki duni.
Kisa cha yote hayo ni madai ya mtoto zawadi kuomba aoneshwe Baba yake
mzazi ili walau aweze kupata pumziko la adha anazo zipata kutoka kwa
ushirika wa ndugu zake hao.Zawadi pamoja na majirani wameuambia mtandao
huu kuwa vitu vilivyo tumika kumwadhibu vilikuwa ni pamoja na nyaya za
simu,mkandaa,na vipande vya chupa katika kumchoma navyo.
Hata hivyo hadi mtandao huu unachapisha taarifa hii watuhumiwa wa
tukio hili yaani Mama mzazi pamoja na Mama mdogo wa Zawadi wanashikiliwa
na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia kwa mahojiano zaidi.
Chanzo: francisgodwin