"SIPO TAYARI KUJIUZULU KWA KUOGOPA MAJUNGU YA VYAMA VYA UPINZANI".....NAIBU WAZIRI WA ELIMU
Victoria
fm ya mjini Mwanza jana asubuhi kipindi cha matukio wameripoti kuwa
wamefanya mahojiano na naibu waziri wa elimu Bw.Philip Mulugo kuhusu
tuhuma zinazomkabili ambapo amesema hawezi kujiuzulu kwa kuogopa majungu
ya vyama vya upinzani wanaopika uongo juu yake ili kuwika kisiasa.
Mulugo
amekanusha madai yote yaliyoandikwa na gazeti la Mwananchi na kudai
kuwa kama kuna mwenye wasiwasi na elimu yake aende akamuoneshe vyeti
vyake vya elimu ya sekondari hadi vya taaluma na chuo alichosoma