Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawala aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua katika kiwanja cha ndege cha arusha.
Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina la Jamal B S, au maarufu kama Bob Sambeke aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro.
Taarifa zaidi zinasema kuwa rubani huyo amefariki muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea na mwili wake umekimbizwa hospitali ya Mount Meru ...
Maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo ni kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja(saa 12.30jioni) kupita.
Kiwanja cha ndege cha Arusha hakina taa za AGL, hivyo huwa kinamaliza au kufunga shughuli zake saa 12.30 za jioni, na hivyo kina'operate kwa masaa 12 tu.Na kawaida ma'controller huondoka baada ya closure ya kiwanja..
Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu