MSANII wa filamu na muziki mwenye mvuto wa aina yake Snura Mushi ‘Snura’,
ameamua kutoa la moyoni kwa madai kuwa sasa anatafuta mwanaume wa
kuweza kufunga naye pingu za maisha lakini kwanza kabisa akubali kumpa
muda mrefu wa kutafuta pesa ili asiwe tegemezi baada ya kuingia ndani ya
ndoa hiyo.
Kauli
ya msanii huyu imekuja mara baada ya mwandishi wetu kumswalika
maswali kadhaa kuhusiana na mikakati ya maisha yake ya muziki
na mahusiano .....
Akiongea
kwa mbwembwe, Snura alidai si kwamba hataki kuolewa bali hataki
kuishi ndani ya ndoa na kuwa tegemezi kwa mwanaume.
“Sitaki kuishi na mwanaume kabla hajakubali kunipa muda wa mimi kutafuta pesa...
Najua anaweza
kuwa na uwezo wa kila kitu lakini hivyo vyote vitakuwa vya kwake na
mimi natakiwa kuwa na mali zangu, lakini bila hivyo nitazeekea kwangu,” alisema.