MESSI, RONALDO NDIYO WACHEZAJI BORA DUNIANI KWASASA - CASILLAS.
NAHODHA wa timu ya taifa
ya Hispania na klabu ya Real Madrid, Iker Casillas amewataja Lionel
Messi na Cristiano Ronaldo kwamba ndio wachezaji bora duniani kwasasa. Golikipa
huyo nyota alikataa kuchagua mchezaji mojawapo kati ya Messi au Ronaldo
ingawa amesema kuwa kama ikimlazimu kufanya hivyo atamchagua Mreno
Ronaldo kwakuwa ndiye anayemfahamu zaidi kutokana na kucheza timu moja. Casillas
aliendelea kusema kuwa ni ngumu kuchagua mchezaji bora kati ya hao
wawili kutokana na ukweli kwamba wote wana uwezo wa hali ya juu. Kauli
ya Casillas imekuja wakati akihojiwa na luninga moja nchini Mexico
ambako walikwenda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya
Puerto Rico Jumatano iliyopita ambapo walishinda mabao 2-1.