HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na  sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.