KIFO CHA KANUMBA CHALIZA WENGI:MATUKIO KATIKA PICHA

 
Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.


Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.


Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefika pamoja na watu mbalimbali.

 Mtandao huu utaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.