JOKATE, DIAMOND SIYO SIRI TENA



Kile kitendawili kwenye Wimbo wa Nimpende Nani wa mwanamuziki Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platinumz,’ kimeteguliwa na sasa siyo siri tena kuwa mkali huyo wa Bongo Fleva anatoka kimapenzi na Miss Tanzania namba 2, 2006/07, Jokate Mwegelo (pichani).

Ama kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Habari inayotamba kwa sasa ni kuwa baada ya kujitahidi kuficha uhusiano wao kwa muda mrefu, mwanzoni mwa wiki hii uzalendo ulimshinda Diamond na kujikuta akiweka kweupe kuwa ni kweli Jokate ni wa kwake.
 
Baada ya Diamond kuweka maneno hayo, ghafla habari hiyo ilisambaa kama moto wa kifuu kwenye mitandao mingi ndani na nje ya Bongo huku ikipokelewa kwa hisia tofauti.
Kuna waliowapongeza na kuisifia ‘kapo’ yao lakini kuna walihoji kuwa mbona walikuwa wakibisha kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi huku Diamond akimuita Jokate dada.

“Watu tuliamini kuwa kitendo cha Jokate kushiriki kwenye video ya Wimbo wa Mawazo wa Diamond ndicho kilichomponza hadi kuhisiwa anatoka na staa huyo, tulidhani anaonewa kumbe ni kweli,” ilisomeka sehemu ya maoni ya mmoja wa watu waliobahatika kuisoma ‘status’ hiyo ya Diamond.