MIMBA YA LULU YATOKA

 
ULE ujauzito wa miezi mitatu wa mwigizaji nyota wa sinema Bongo ambaye kwa sasa yuko nyuma ya nondo za Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa kesi ya kifo cha Steven Kanumba, Elizabeth Michael 'Lulu' umedaiwa kuchoropoka
 

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ambacho ni makini, sababu kubwa ya mimba hiyo kutoka ni kutunga nje ya mfuko wa uzazi hali ambayo ingemletea matatizo Lulu.

“Nikwambie kitu, unajua wengi wanaamini Lulu ana mimba na hivi karibuini iliandikwa imefikisha miezi mitatu, ilikuwa sahihi, lakini ukweli ni kwamba kwa sasa imetoka.

“Sababu kubwa ni kwamba afya yake ilidorora, ukiachia ule ugonjwa wa U.T.I alioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anao, lakini kingine ni kuwa iligundulika ujazuito wake ulitunga nje ya mfuko wa uzazi ikawa haina jinsi, ikabidi kutolewa na kusafishwa,” kilisema chanzo hicho bila kuainisha tukio hilo lilitokea lini.


Kikiendelea kuzungumza kwa umakini mkubwa, chanzo chetu kilidai kuwa eti ujauzito huo ni wa tatu kuchoropoka kwa msanii huyo.

“Unajua huu unakuwa ujauzito wa tatu kwa Lulu kutoka. Kwa kweli kama si hivyo angekuwa na mtoto,” kilisema chanzo bila kuweka wazi nyingine mbili zilitoka kwa matatizo gani. 

“Kuna wakati Lulu alikwenda China, aliporudi alikuwa na ujauzito, lakini nao ulitoka, inaonekana ana matatizo kidogo kwenye upande wa kizazi,” kilidai chanzo hicho.

Kikaendelea: “Baada ya hapo, haukupita muda mrefu, akanasa nyingine ya mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva, pia hiyo nayo ikaja kutoka ya tatu ni hii ya Kanumba.”


SOURCE: Global Publisher