Lugha kama hizi zimesababisha Watanzania wengi wakose hamu ya kusikiliza vikao
vya Bunge.
Tumechoshwa na lugha chafu za waheshimiwa. Bunge ni sehemu ambayo tulipaswa kuwa
tunasikiliza hoja za sera zikiwasilishwa na sheria kutungwa, lakini
imeshindikana.
JOSEPH MBILINYI:
Hatuwezi kuwa na WAZIRI WA ELIMU BOYA mwenye elimu ya kuunga unga halafu tufanye vizuri katika sekta ya elimu , haiwezekani."
LIVINGSTONE LUSINDE:
"Siwezi kuikubali taarifa
hiyo.Nadhani huyu mtu bado amechanganyikiwa na uchaguzi wa
kenya.Mimi sijaitaja Chadema bali nimesema kuna chama kimoja cha
siasa,SIJUI YEYE ANAWASHWA NINI..!!
JUMA NKAMIA:
Sugu naomba unyamaze.Mimi ndiye nazungumza.Mimi siongei na mbwa,naongea na mwenye mbwa.
Khatibu Saidi Haji (Konde - CUF)
Alimtukana
Freeman Mbowe mbunge wa Hai kwa kusema "Mbowe kaja hapa anajambajamba
tu" akilalamikia hoja ya Mbowe kuhusu idadi ya watu wa visiwani. Alimtukana Mchungaji Msigwa: "Wewe Msigwa ni mchungaji wa watu au mchungaji wa nguruwe? "Alitoa tusi hilo kutokana na Mchungaji Msigwa kutoa kauli ya kwamba Zanzibar kuna udini.