Lulu Atishia Kunywa Sumu, Azuiliwa Kuuaga Mwili wa Kanumba

MSAANII wa filamu Elizabeth Michael [Lulu] ombi lake la kutaka kwenda kuuaga mwili wa Kanumba limezuiliwa kwa kile kilichodaiwa kisheria hawezi kufanya hivyo, Lulu amedai anataka kuthibitisha kama kweli Kanumba amefariki ili anywe sumu apotee duniani. Elizabeth Michael maarufu kama Lulu aliliomba jeshi la Polisi nchini wamuachie kwa dakika kadhaa kwenda kuuaga mwili huo ili aweze kuhakiki kama ni kweli Kanumba amefariki dunia.


Lulu hadi sasa ni mtu pekee anayehusishwa na kifo cha Kanumba kwa kuwa dakika chache kabla ya kifo hicho alikuwa na marehemu nyumbani kwake Vatican Sinza jijini Dar es Salaam.

Lulu anawaomba Watanzania msamaha kwa kuhusishwa na kifo hicho na haelewi ilikuwa vipi hadi Kanumba amepoteza maisha kitendo ambacho kinamsikitisha na kumkosesha raha.

lulu ameomba apewe muda wa kuthibisha kweli Kanumba amefariki dunia na ili na yeye anywe kunywa sumu ili apoteee duniani hapa.

Hadi sasa Lulu anaendelea kushikiliwa na polisi kituo cha polisi cha Oysterbay.

Jana jopo la madaktari lilianza kuuchunguza mwili wa aliyekuwa mcheza filamu maarufu nchini, Steven Kanumba, kwa lengo la kubaini sababu zilizosababisha kifo chake kilichotokea Jumamosi iliyopita majira ya alfajiri akiwa nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema taarifa kuhusiana na uchunguzi huo itatolewa na madaktari baada ya kukamilika.