Madee apigwa ‘wanted’ Arusha, haruhusiwi kukanyaga ardhi yake


Kama ilivyozoeleka kwa ndugu zetu wa Arusha ni kwamba ukimess up na chalii mmoja wa Arachuga tena anayekubalika, tambua kuwa umemess up na mji mzima.

We saw it coming by the way! Kwamba baada ya Madee kudaiwa kumzingua Dogo Janja kiasi cha kumfanya arudi nyumbani kwao wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa story kutoka A-TOWN ni kwamba kama Madee asipoonyosha maelezo yake kuhusu haki ya Dogo Janja ama kuomba radhi kwa walichomfanyia (Tip Top Connection), Arusha itakua chungu kwao. Kuna wale wanaosema kuwa wakimwona Arusha basi atarudi Dar jina tu.
Wapenzi wa hip hop jijini Arusha wana hasira na Madee kwakuwa wanaamini kuwa amemdhulumu Dogo Janja haki yake na kama asipoenda hewani kukiri kosa lake mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwake.
Juzi Dogo Janja alifanya show yake ya kwanza bila kuwa chini ya uongozi wa Tip Top Connection baada ya kupewa shavu na Airtel iliyokuwa inazindua kampeni yake ya Super5.
Mashabiki wa muziki jijini humo walifurahia show yake, hali inayoashiria kuwa wako nyuma yake no matter what!