Dudu Baya aelezea sababu za kumpiga mtangazaji wa Kiss Fm


Wiki iliyopita tuliandika habari kuhusu rapper Dudu Baya kumpiga mtangazaji wa kituo cha radio cha Kiss FM, Ezden Jumanne aka The Rocker baada ya kumnyima show.


Jana Clouds Fm kupitia kipindi cha XXL wamemhoji msanii huyo ambaye amesema sababu za kumpiga mtangazaji huyo ni kuwa alipofika Mwanza kwa mara ya kwanza aliitisha kikao cha wasanii wote wa jiji hilo ili kupanga mikakati ya kukuza muziki.
Kutokana na kikao hicho, Dudu anasema walianzisha chama walichokipa jina la ‘Mwanza Kwanza.’
Anasema miezi kama mitatu iliyopita alifariki rapper wa Mwanza aliyekuwa anaitwa Mo Chella kwa kuchomwa na kisu na ndipo Ezden aliandaa show ya kuchangisha fedha za kuisaidia familia ya marehemu bila kumshirikisha Dudu Baya.
Kutokana na kitendo hicho uhusiano kati yake na Ezden uliingia kasoro kiasi cha kutozungumza vizuri kila wanapokutana na ndio maana hivi karibuni alifikia hatua ya kumpiga.
Hata hivyo Mpekuziblog imefuatilia habari hii na kubaini kuwa chama hiki cha Mwanza Kwanza kilianzishwa miaka minne iliyopita hata kabla ya Dudu Baya kuhamia Mwanza.
Mwanza Kwanza iliyoanza kama familia ya hip hop ilianzishwa na msanii aitwaye Athuman Mohamed aka Flexible mwaka 2008 ikiwa na wasanii watano ambao ni Star J, Sam, Goba, Dachi na yeye mwenyewe.


“Kuna watu walipoona mafanikio yameanza kuja na familia inakuwa kubwa na kujulikana wakaanza kuingilia na mwisho wa siku wanasema ni ya kwao na wao ndio walioianzisha. 


Watu hao ni Kabago na wafuasi wake na Dudu Baya na watu wake mpaka wanaleta mgawanyiko cause hawajui mwanzo na malengo yetu ya kuunda hiyo familia,” anasema Flexible.

“Wanagombana wakati hakuna hata mmoja anayehusika na wahusika ni sisi wana Mwanza Kwanza.”
Flexible ameendelea kusema, “ Dudu ndio msanii aliyefeli kuzidi underground wote wa Mwanza na ndio anajaribu kurudi lakini hata studio anazofanyia ni local sana. Anapiga show za vijijini na wanasema hata huko hajazi, inshort amefulia sana.”