Elizabeth Michael "Lulu" alisoma shule ya sekondari "Perfect Vision" hapo zamani katika masomo yake ya O level.
Habari za kuaminika ni kwamba wanafunzi wa shule hiyo wameamua kujichangisha wenyewe ili wapate pesa za kumsaidia Lulu kwenye suala la kisheria.
Wanafunzi hao wamelaani kitendo cha kesi yake kupelekwa mbele kila inapoitwa na kufanya gharama izidi kuongezeka.
Chanzo chetu kiliongea na mkuu wa shule hiyo na alikuwa na haya:, "NI kweli wanafunzi wangu kwa ridhaa yao wenyewe wameamua kumchangia mwenzao ambaye alisoma hapa miaka kadhaa iliyopita"