DR. HARRISON MAKYEMBE AKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA USAFIRISHAJI

Sakata la kupandisha nauli kwa mabasi yaendayo mikoani katika kituo kikuu cha Ubungo jijini Dar es Salaam, limemlazimu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kukutana na wadau wa sekta ya usafirishaji.
Dk. Mwakyembe jana alikutana na Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (Taboa) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Jumatatu wiki hii, Dk. Mwakyembe alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo na kuendesha operesheni ya kukamata magari yanayotoza nauli kubwa kinyume cha sheria ambapo yalipigwa Faini ya Sh. 250,000 kwa kila kosa.