MASANJA MKANDAMIZAJI ATOFAUTIANA NA WASANII WENGINE KUHUSU ALBUM.

Masanja.
Tofauti na wasanii wengine wa Tanzania ambao hutangaza kuwashitaki au kuwachukulia hatua wezi wa album/kazi zao wanapobainika, Masanja amekua msanii wa kwanza kumsikia na msimamo tofauti kuhusu hiyo ishu ya wizi.
Masanja ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili, ametoa album yake ya kwanza tayari inaitwa Hakuna jipya chini ya jua.
Baada ya kutangaza kukamilika kwa hiyo album,  amesema “nimemaliza kufanya album yangu ya Gospel najua wako watu mamasta wa kuburn kazi za waimbaji nimewakaribisha waburn hii yangu, yani hamna kesi hashikwi mtu atakaeburn kazi yangu kwa sababu hii ni huduma ukiburn wauzie watu hata mia mia usiziweke ndani”
 
Kwenye sentensi nyingine Mchekeshaji huyu wa Orijino Komedi ya TBC1 amesema “kuna watu wananiambia Masanja tumeona watu wanauza CD feki nasema kama na wewe unaweza nunua na  ukatengeneze zako kwa sababu hii ni huduma nataka watu wapate ujumbe huu wabadilike wamjue Yesu tunaemuhubiri mwanawane”