Mtandao wa Thunderumblings wampa ushauri Hasheem Thabeet
Jana ilibainika wazi kuwa mtanzania Hasheem Thabeet amesaini mkataba wa kuichezea timu ya Oklahama City Thunder kwaajili ya misimu miwili ya ligi ya NBA ambapo kwa mwaka atakuwa akilipwa dola 880,000.
Hata hivyo tangu Hasheem aanze kucheza kwenye ligi ya NBA, hajawahi kuonesha kiwango cha kuridhisha na hivyo kujikuta akikoselewa mara nyingi na waandishi wa Marekani.
Hata hivyo mwandishi wa mtandao wa ThunderRumblings uliojikita katika kuandika habari za timu mpya ya Hasheem, Darnell Mayberry amempa ushauri wa kumsaidia mchezaji huyo kama anavyasema:
“Sio rahisi kwa Thabeet kuingia uwanjani mara nyingi msimu ujao. Kitu muhimu kwa Thunder, na Thabeet, ni kufocus kwenye maendeleo.
Ni wazi, kuna kipaji ndani ya urefu wa Thabeet wa 7-foot-3. Hakuwa mchezaji bora wa mwaka wa defense kwa misimu miwili na Co-Big East Player of the Year kwenye msimu wa mwisho wa UConn bure.
Lakini huu ni muda sasa wa kukitumia kipaji hicho. Ni muda wa Thabeet kufanya kazi.
Hii itakuwa ni timu ya nne kwa Thabeet ndani ya misimu minne baada ya kuwa drafted kama mchezaji wa pili kwenye usajili mwaka 2009. Tunaamini kuwa hii ndo itakuwa ni nafasi ya mwisho kuthibitisha kuwa anastahili kuwepo kwenye ligi ya NBA.
Lakini kitu cha kwanza ambacho Thabeet anatakiwa kufanya kuonesha kuwa muda huu, timu hii itakuwa tofauti na misimu mitatu iliyopita ni kwenda Orlando kuungana na wachezaji wenzake wapya kwenye summer league.
Mara nyingi wachezaji maarufu huwa hawashiriki kwenye ligi hii. Lakini katika mtu ambaye anatakiwa kujifanya mjinga ni Thabeet. Kama mimi ningekuwa Thabeet, ninajitolea kwenda na kushindana badala ya kusubiri kocha aniambie niende.
Ni kitu rahisi kuweka ‘good first impression’ na kuprove kuwa yaliyopita, yamepita. Uthibitisho kuwa sasa yupo tayari kufanya kazi kwa bidii na kufanya kinachotakiwa kustawi kuwa mchezaji ambaye wengi waliamini alikuwa na sifa za kuwa.
Iwapo hakuna kingine. Ni nafasi ya kucheza. Na Mungu anajua Thabeet anahitaji hilo.
Kwenye misimu minne iliyopita, Thabeet amecheza kwa dakika 512 pekee. Kwa kulinganisha, mchezaji (guard) chipukizi wa Thunder Reggie Jackson alicheza dakika 501 msimu huu. Ukitengenisha muda wake akiwa na Houston na Portland mwaka huu, Thabeet alicheza dakika 139 tu. Kevin Durant alicheza dakika 213 kwenye fainali za NBA dhidi ya Miami pekee.
Muda wa uwanjani ndicho kitu anahitaji Thabeet kuliko kingine chochote. Kama hatocheza, ama kutokuwa mchezaji aliyetegemewa kuwa defender mzuri, basi na iwe. Lakini kuna njia moja ya kutoka.
Thabeet anahitaji kuchukua hatua hiyo ya kwanza. Anahitajika kwenda Orlando.”