SPAIN VS ITALY EURO 2012 FINAL: WATU MILLIONI 250 KUANGALIA, TIKETI MOJA INAUZWA NI HATARI - NI BALOTELLI AU TORRES NANI KUONGEZA TAJI USIKU WA LEO - YAJUE MAMBO MUHIMU KUHUSU FAINALI HII

1: Hii ndio fainali ya kwanza yaEuro ambayo magolikipa wote watakuwa manahodha.

2: Ikiwa Spain wakishinda leo, Vicente Del Bosque atakuwa kocha wa kwanza wa timu ya taifa kushinda kombe la dunia na kombe la ulaya. Helmut Schon aliongoza Ujerumani Magharibi kushinda Euro 1972 na kufuatia na kombe la dunia 1974.



6: Goli la haraka zaidi kufungwa kwenye fainali ya Euro liliwekwa kimiani na mchezaji wa Spain Jesus Pereda dakika ya sita ya mchezo wa fainali.

7: Wachezaji saba tu kutoka nje ya ligi ya Spain na Italy ndio wapo kwenye vikosi vya timu hizi mbili.

7: Kutakuwa na redio saba za kihspaniola zitakazotangaza mchezo wa leo, nyingi kuliko nchi yoyote dunaini.

10: Mreno Pedro Proenca ndio atakuwa mwamuzi wa fainali ya leo jumapili na ameshatoa kadi 10 za njano, huku akiwa hajaigusa kadi nyekundu kwenye michuano hii.

15: Italy wameshapata kadi za njano 15 kwenye Euro 2012, nyingi kuliko timu yoyote kwenye michuano hii.

17: Alvaro Arbeloa ndio mchezaji aliyecheza faulo nyingi kuliko wote kwenye mashindano, akicheza faulo mara 17.

27: Huu ndio wastani wa umri wa kikosi cha Spain.

28: Huu ndio wastani wa umri wa kikosi cha Italia - miaka 28.

31: Kutakuwepo na camera 31 zitakazokuwa zikinasa picha za matukio ya mchezo wa leo kwenye uwanja wa Olympic.

55: Italy wamepiga mashuti 55 kwenye lango - mengi kuliko timu yoyote kwenye Euro 2012.

92.8: Kiwango cha pasi zilizofika cha Xavi ni asilimia 92.8, kiwango kikubwa kuliko mchezaji yoyote kwenye mashindano haya na mchezaji yoyote kwenye fainali ya leo.

120: Gianluigi Buffon atacheza mechi yake ya 120 kwa Italy - ikiwa atapangwa kwenye fainali ya leo.

137: Buffon bado hajamfikia mpinzani wake kwenye fainali ya leo Iker Casillas ambaye amecheza mechi 137 akiwa na La Roja.

164: Mshambuliaji wa Italy Sebastian Giovinco ndio mchezaji mfupi zaidi kwenye Euro 2012 - akiwa na sentimita 164.

180: Huu ndio uwiano wa urefu wa wachezaji wa Spain

181: Huu ndio uwiano wa urefu wa wachezaji wa Italia.

200: Fainali hii itaonyeshwa kwenye zaidi ya nchi 200 duniani.

455: Xavi pekee amepiga pasi zilizofika 455 - nyingi kuliko mchezaji yoyte kwenye Euro 2012.

2000: Adidas wametoa mipira 2000 kwa ajili ya mechi za michuano hii.

3, 568: Gharama ya tiketi ya bei ya katikati kwa ajili ya mchezo wa fainali ni €3468

40,000: Kiungo wa Italia Andrea Pirlo anamiliki kampuni ya kutengeneza wine, Pratum Coller, ambayo inauza zaidi ya chupa 40000 kwa mwaka.

68,055: Kutakuwa na watu 68055 ndani ya uwanja wa Olympic mjini Kiev kwa ajili ya kuangalia fainali ya leo.

582,810: Wachezaji wote wa Spain wamekimbia mita zipatazo 582,810 kwenye Euro 2012.

605,020: Wachezaji wote wa Italy wamekimbia mita zipatazo 582,810 kwenye Euro 2012.

1,000,000: Zaidi ya watu million moja wamenunua jezi ya juu ya Spain zilizotengenezwa na adidas kwa ajili ya Euro 2012.

1, 000,000 - Kampuni ya vinywaji ya Carlsberg inategemea kuuza vikombe millioni moja vya bia kwenye dakika 15 za mapumziko kwenye uwanja wa Olympic na maeneo mengine yaliyotengwa maalum kwa ajili kuangalizia mpira wa mechi ya fainali mjini Kiev.

1, 320,000 - Idadi yote ya mashabiki ambao wameingia viwanjani kuangalia Euro 2012 imefika watu millioni 1.32.

250,000,000 - Watu millioni 250 wanategemewa kuangalia mechi ya fainali ya leo duniani  kote.