Tanzania Yapewa Msaada Wa Euro Milioni 126.5 Na Jumuiya Ya Ulaya

Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jose Manuel Barroso wakishuhudia utiaji saini makubaliano ya msaada wa fedha Euro milioni 126.5, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Utiaji saini ulifanywa na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa (kulia) na Mjumbe wa Maendeleo wa EU, Andris Piebalgs (kushoto). Msaada huo ni kwa ajili ya matengenezo ya barabara zaidi ya Kilometa 200, upatikanaji wa maji kwa watu 500,000 na kuimarisha mfumo wa maji na usafi kwa watu 140,000 Tanzania.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Jose Manuel Barroso Ikulu jijini Dar es Salaam State leo.


Rais Jakaya Kikwete (Katikati kushoto) akiongoza ujumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo na ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ulioongozwa na Rais wa EU, Jose Manuel Barroso, Ikulu jijini Dar es Salaam