Miili ya wakimbizi hao ikiteremshwa katika makaburi ya Kolla kutoka kwenye lori.
Kiongozi wa dini ya Kikrsto akishiriki mazishi hayo.
Kiongozi wa dini ya Kiislam aliyeshiriki mazishi hayo.
Mwili ukiwa kaburini.
Mwili ukitayarishwa kuteremshwa kaburini.
Mazishi yakiendelea.
WAKIMBIZI 127 wa Ethiopia waliokuwa
wakisafiri kwa kificho kutoka Ethiopia kwenda nchi za Malawi na Afrika
Kusini kwa lengo la kusaka maisha bora baadhi yao walipoteza maisha
hivi majuzi baada ya kukosa hewa wakati wakisafirishwa kwenye kontena
ili kuwakwepa maofisa wa Idara ya Uhamiaji nchini.
Tukio hilo lilitokea katikati ya wiki hii mkoani Dodoma ambapo Wasomali 43 waligundulika kuwa wamekufa na 84 wakiwa wamenusurika.
Miili hiyo iliyokuwa imeanza kutoa harufu, 22 ilizikwa Dodoma na 21 ilizikwa Ijumaa wiki hii mjini Morogoro katika makaburi ya Kolla ilikopewa mazishi ya jumla ya Kikristo na Kiislam.

(PICHA/HABARI: DUNSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO)