Neema Kumba (kushoto) akipokea fomu ya kuwania nyadhifa hizo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma,
KADA
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa (UVCCM) na
Msomi wa digrii ya uchumi, Neema Kumba amejitosa kwenye uchaguzi mkuu
wa umoja huo Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na uwakilishi
UWT.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Ijumaa Agosti 3 jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma,
Kumba ambae awali alikua Katibu wa CCM, tawi la North
London, Nchini Uingereza,alipokua akichukulia digrii yake ya uchumi,
alisema lengo ni kuakikisha mikakati thabiti inajengeka kwa kiwango
kikubwa miongoni mwa vjana na wanawake wote nchini.
“Kwa
umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu
ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia
wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua
wakisahauriwa na huu ndio wakati wa kuwainua” alisema Kumba.
Mbali
na kuchukua fomu hiyo ya NEC na uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari
alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.
Mpaka
sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM, wamejitokeza kuchukua fomu
za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu hizo, Agosti 6.