CAZORLA ATUA RASMI ARSENAL.

Santiago Cazorla.
KLABU Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa a Hispania, Santiago Cazorla kutoka klabu ya Malaga. Cazorla mwenye umri wa miaka 27 alithibitisha suala hilo baada ya kuandikia mashabiki wake katika mtandao wa kijamii wa twitter kwamba kwasasa yeye ni mchezaji wa Arsenal. Cazorla ambaye amecheza michezo 47 katika timu ya taifa ya Hispania alikosa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa hernia lakini alirejea tena uwanjani na kuiwezesha klabu yake ya Malaga kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kiungo huyo alikuwepo katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kilinyakuwa taji la Ulaya mapema mwezi uliopita na pia alikuwepo katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kilinyakuwa taji hilo mwaka 2008. Taarifa zisizo ramsi zinasema kuwa Arsenal imemsajili kiungo huyo kwa ada ya paundi milioni 20 huku pia wakitaka kumsajili kwa mkpo kiungo wa Real Madrid Nuri Sahin.