MENEZES AMUONDOA HOFU GANSO.

Ganso.
KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil inayoshiriki michuano ya Olimpiki, Mano Menezes amesema kuwa amefurahishwa kuona kiungo wa timu hiyo Paulo Henrique Ganso akitabasamu tena baada ya madaktari kumruhusu kuendelea na mashindano hayo pamoja na maumivu ya mguu wake wa kushoto yaliyokuwa yakimkabili. Menezes amesema kuwa Ganso ataendelea kuwa sehemu ya kikosi chake na pengine anaweza kuwemo katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Honduras utakaochezwa kesho jijini Newcastle. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa madaktari wa timu hiyo walikuwa hawana uhakika ni kwa kiasi gano Ganso alikuwa ameumia mpaka alipofanyiwa vipimo na kugundua kuwa tatizo halikuwa kubwa sana. Katika michezo miwili ambayo Brazil imecheza katika michuano hiyo Ganso amekuwa akiingia kutoka benchi la wachezaji wa akiba kabla ya kukosa mchezo wa tatu kwasababu ya maumivu ya msuli yaliyokuwa yakimsumbua.