RC Iringa: Sensa Ni Zaidi Ya Kuhesabu Watu


Waandishi wa Habari wakiwa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt.hristine Ishengoma (wa tatu kati kati waliokaa) Chuo kikuu cha ruaha Manispaa ya Iringa.
Na Hakimu Mwafongo
SENSA ya watu na makazi ni zaidi ya kuhesabu watu bali ni bali ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kusambaza takwimu za kijiografia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao kwa kipindi maalumu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma kwenye semina ya waandishi wa habari wa mikoa ya nyanda za juu kusini ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Njombe, Lindi na Mtwara yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo kikuu cha Ruaha Manispaa ya Iringa.

“Sensa haina maana kuhesabu watu tu bali mambo mengi yakiwemo ukusanyaji wa taarifa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii katika kuharakisha maendeleo ya wananchi”, alisema.
Alisema zoezi hilo lina lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsi, mahali wanapoishi, hali yao ya kielimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi.

Dkt. Ishengoma alisema taarifa hizo zitatumika kusaidia kutathimini Dira ya maendeleo ya mwa 2025, Zanzibar 2020, Mkakati wa Kupunguza na Kukuza Uchumi Tanzania (MKAKATI) na Malengo ya Milenia (MGDs).

Aidha Mwanasheria kutoka Taasisi ya Takwimu Tanzania, Osea Mangula alitahadharisha mtu au kundi la watu linalotaka kukwamisha zoezi la sensa kuwa watachukuliwa hataua za kisheria ikiwemo kushitakiwa na Jamhuri.

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba aliwataka watanzania kuwashirikisha wenye ulemavu na vikongwe wote pasipo kuwaficha majumbani mwao.