SHUJAA WA OLIMPIKI MO FARAH ASONONESHWA KUONDOKA RVP ARSENAL.

MWANARIADHA shujaa wa mbio za Olimpiki zilizofanyika jijini London ambaye ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya Arsenal Mo Farah ameeleza masikitiko yake baada ya mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Robin van Persie kuhamia Manchester United. Farah mwenye miaka 29 ambaye ni mshindi wa medali mbili za dhahabu za olimpiki katika mbio za mita 10,000 na 5,000 amesema kuwa pamoja na kusikitishwa kuondoka kwa mchezaji huyo lakini amemuelewa kwa uamuzi wake akiwa kama mwanamichezo. Mwanariadha huyo raia wa Uingereza mwenye asili ya Somalia aliendelea kusema Van Persie anahitaji mataji ndio maana ameamua kuhama na hilo ni jambo la kwawaida katika mchezo wa soka tofauti ilivyo katika riadha na anadhani aliona ni vigumu kupata mafanikio hayo akiwa katika klabu hiyo. Farah amesema akiongea kama mshabiki amehuzunishwa sana Arsenal kumkosa mchezaji wa kiwango kama cha Van Persie.