Fumanizi hilo lilibuliwa na gazeti hili, Septemba 18, mwaka huu
ambapo Judith Lekule na mume wa mwanamke aliyetambuliwa kwa jina moja la
Pendo walinaswa chumbani wakiivunja amri ya sita ya muumba.
Kwa mujibu wa vyanzo, Judith yu mbioni kwenda kortini kwa lengo la kumfungulia mashitaka Pendo akidai alimdhalilisha kwa kudai alimfumania akiwa na mumewe.
“Kuna watu wanamshawishi Judith eti asikae kimya, aende mahakamani akamshitaki Pendo kwamba alimdhalilisha kusema alimfumania na mumewe,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, vyanzo vimeeleza kwamba, Judith anashindwa kuutumia ushauri huo kutokana na ukweli kwamba, kesi hiyo inaweza kumgeukia mwenyewe kwa sababu yeye ndiye aliyefumaniwa.
Sambamba na madai hayo, inasemekana pia kwamba mtaani anapoishi Judith kumekuwa kuchungu kwake baada ya baadhi ya watu kutumia habari ya kwenye gazeti kumkejeli na kumuonya akome kuwadandia waume za watu kwani si tabia nzuri.
“Hali hiyo ya kunyooshewa vidole na watu inamnyima raha Judith, anashindwa kutembea kwa uhuru mitaani,” alisema mnyetishaji wetu.
Nao baadhi ya marafiki wa kike wa Judhith wamehuzunishwa na kitendo cha mwenzao kufumaniwa na kupewa kipigo.
Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, ndugu wamemtaka Judith aondoke anapoishi kufuatia kitendo alichokifanya ikielezwa ameitia aibu familia.
Kwa upande wake, Pendo ameeleza kwamba mumewe alimuomba msamaha na amemsamehe, yameisha pia akasema baada ya lile fumanizi, Judith amemfuata nyumbani kwake mara mbili kwa lengo la kuomba msamaha.
“Cha ajabu sasa amegeuka na kutoa vitisho, Judith ni rafiki yangu, anajua alichokifanya ndiyo maana hata wapambe wake wanamshawishi akanishitaki lakini moyo wake unakuwa mgumu,” alisema Pendo.
Habari za kufumaniwa kwa Judith zilitolewa katika gazeti hili toleo namba 727 la Septemba 20-26, 2012 likiwa na kichwa kisemacho
UWAZI