Akiojiwa na mwandishi baada ya kukamatwa
.MREMBO mmoja, Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar amebambwa
akidaiwa kuiba fedha kwa njia za miujiza eneo la Bunju Mwanjenje kwenye
duka la Wapemba.Imeelezwa kuwa katika tukio hilo, Rukia alichukua fedha kimiujiza
dukani na kutokomea, hali iliyosababisha wenye duka kutangaza dau la
shilingi 500,000 kwa atakayewezesha kukamatwa kwake.wakimtaka amtaje aliyemtuma.
Baada ya kupokea kichapo, mrembo huyo aliwataja baadhi ya watu akiwemo mganga mmoja anayetokea Sumbawanga (jina tunalo)
na kudai kuwa ndiye aliyekuwa akimpa dawa (chuma ulete).
“Dawa hiyo huwa naiweka kwenye pesa zangu nyumbani ili ziongezeke na nyingine huwa natembea nayo kwa ajili ya kujipatia pesa,” alisema mrembo huyo.
Mrembo huyo alikiri kufanikiwa kuiba mamilioni ya shilingi kwa kutumia dawa hiyo na kuomba asamehewe. Rukia aliokolewa na ndugu zake pamoja na wasamaria wema waliompeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo alikofunguliwa mashtaka ya wizi.
Tukio hilo ni la pili kwa Rukia kwani mara ya kwanza alikamatwa Tabata jijini Dar es Salaam miezi michache iliyopita kwa tuhuma kama hizo lakini akaachiliwa baada ya kuomba msamaha.
chanzo tuangaze.blogspot.com