
 Siku Mwanahabari  Daudi  Mwangosi  alivyouwawa  kwa  bomu 
ASKARI,
   Pacificus Cleophace Simon (23) anayedaiwa kumuua Mwandishi wa   
Television ya Chanel Ten mkoa wa Iringa, Daudi Mwangosi amefikishwa   
mahakamani     
Simon
   aliyetambuliwa kwa namba G2573 mkazi wa FFU Iringa alifikishwa 
mahakamani   hapo chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu na waliovaria 
sare wakiwa  na  siraha zaidi ya 10.   
Pia walitumia gari aina ya Land Cruser (Shangingi) nyeupe yenye namba za usajili T320ARC likisindikizwa na Land Cruser pic up.   
Mbele
   ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama wa wilaya, Dyness Lyimo,   
Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mkuu, Michael Luwena alisema inadaiwa   
kuwa Pacificus Cleophace Simon alitenda kosa hilo Septemba, 2 mwaka huu 
  eneo la Nyololo wilayani Mufindi.   
Kesi
  hiyo ya mauaji imefunguliwa chini ya kifungu 196, kanuni za adhabu  
sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002, Kwa mujibu wa kesi za mada mtuhumiwa  
hakurusiwa kujibu chochote.   
Hakimu
   Mkazi Mwandamizi wa Mahakama wa wilaya, Dyness Lyimo alisema mahakama
   haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji hivyo ni kusoma  tu.Kesi 
hiyo itatajwa tena Septemba 26, mwaka huu.  
 
