MAN UNITED YAMTENGEA NEYMAR PAUNDI MILIONI 38.

KLABU ya Manchester
United imetenga kitita cha paundi milioni 38 kwa ajili ya kumnyakuwa
mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar. Dau hilo ambalo
linavunja rekodi ya klabu hiyo, ilishindwa wakati timu hiyo ilipomtaka
mara ya kwanza baada ya nyota huyo mwenye miaka 20 anayecheza katika
klabu ya Santos kusema kuwa anataka kubakia katika klabu yake hiyo mpaka
baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 ambapo nchi yake itakuwa
wenyeji. Nia ya meneja wa United Sir Alex Ferguson kutaka kumsajili
Neymar kunazua maswali mengi juu ya mustakabali wa mshambuliaji wa klabu
hiyo Wayne Rooney kwani kocha huyo ameonekana hawezi kushindwa kujaribu
kumsajili Neymar tena katika kipindi cha dirisha dogo la usajili
Januari mwakani. United imeamua kuhamishia nguvu zake kwa Neymar baada
ya kuzidiwa kete na klabu ya Paris St Germain ya Ufaransa katika mbio za
kumsajili Mbrazil mwingine Lucas Moura ambaye ana umri wa miaka 19. Ila
bado inaonekana kutakuwa na vita kubwa ya kumgombani mchezaji huyo
ambaye amefunga mabao 113 katika michezo 190 aliyochezea klabu ya
Santos, kwani klabu za Real Madrid na Barcelona nazo zimeonyesha nia ya
kumsajili.