Pinda Awavua Madaraka Wakurugenzi Sita


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewavua madaraka wakurugenzi sita wa Halmashauri za Wilaya kwa kushindwa kusimamia rasilimali watu, fedha na kutowajibika.Kutokana na hatua hiyo, Waziri Mkuu Pinda amewateua watu sita kukaimu nafasi hizo na wakurugenzi wapya 14 huku akiwahamisha wakurugenzi 27 kutoka katika vituo vyao vya kazi kwa sababu mbalimbali.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia, alisema wakurugenzi hao walivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia rasilimali watu na fedha, kusababisha halmashauri kupata hati chafu na uzembe.


Aliwataja wakurugenzi hao waliovuliwa madaraka kuwa ni Willy Njau (Mwanga), Mpangalukela Tatala (Geita), Theonest Nyamhanga (Kishapu), Eden Munisi (Morogoro), Mhando Senyagwa (Kyela) na Nicholaus Kileka (Ngorongoro).


Pia alisema Serikali haitasita kuchukua hatua pale inapobidi ili kuboresha utendaji, na kwamba wengine tayari wana kesi na si busara kuwe na mtu anayekaimu zaidi ya miaka mitatu.


Pia alisema hatua za kinidhamu bado zinaendelea na kwamba baadhi ya wakurugenzi hao tayari wamewafikisha kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya hatua zaidi.


Waziri huyo aliwataja wakurugenzi wapya walioteuliwa kujaza nafasi hizo kuwa ni Abdalah Kidwanka (Geita), Rutius Bilakwata (Kishapu), Naomi Nko (Magu ), Abdalah Mfaume (Kyela), Twalib Mbasha (Monduli), Henry Ruyagu (Urambo), Adam Mgoyi (Mbarali) na Estomih Chang’a (Mpanda).


Wamo pia Leti Shuma (Mwanga), Mohamed Maje (Namtumbo) Fulgency Mponji (Moshi), Robert Nehata (Tunduru), Isabela Chilumba (Kahama), Fikiri Malembeka (Sengerema), Paul Malala (Njombe) na Nasib Mbaga (Biharamulo).


Wakurugenzi wanaohamishwa ili kujaza vituo wazi ni Bibie Mnyamagola (Kongwa), Daudi Mayeji (Kilindi), Protace Magayane (Nkasi), Saada Mwaruka (Mkuranga), Sipora Liana(Tabora Manispaa), Hadija Makuwani (Wilaya ya Tabora), Doroth Rwiza (Kasulu).


Wengine ni Kelvin Makonda (Manispaa ya Lindi), Pudenciana Kisaka (Iringa), Tina Sekambo (Makambako), Beatrice Dominick (Masasi), Gladyness Ndyamvuye (Bukoba), Nathan Mshana (Ngorongoro), Cornel Ngudungi (Ngara), Mohamed Mkupete (Mtwara Manispaa), Dk Koroine Ole Kuney (Misungwi).


Wamo pia Ephraem Ole Nguyaine (Rorya), Goody Pamba (Igunga), Fidelis Lumato (Ludewa), Athuman (Tarime) na Ahmad Sawa (Musoma Manispaa).


Waliohamishwa kwenda kwenye halmashauri mpya ni Magreth Nakainga (Geita), Eliza Bwana (Bariadi), Zuberi Mbyana, Ilemela Manispaa (Biharamulo), Mohamed Nanyanje (Masasi), Erica Musika (Kahama), Imelda Ishuza (Busokelo).


Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari