Mtandao
wa Ghafla wa nchini Kenya jana uliandika habari inayodai kuwa huenda
msanii wa Tanzania aliyetajwa kwenye tuzo za Channel O 2012, Ambwene
Yesaya, akahamia jijini Nairobi, Kenya.
“Seeing
that Nairobi is kind of like the center of all showbiz matters in East
Africa, AY has seen it convenient and advantageous to set up shop here
in Nairobi. According to sources, AY was actually looking for a vacant
office days before he left for his country.
Could he be the next artist to relocate to Kenya? I sure hope so,” uliandika mtandao huo.
Mwandishi aliamua kumpigia simu AY ili kumuuliza kama kweli ana mpango wa kuhamia nchini Kenya na kufungua duka.
“Unajua sehemu unaenda sana sana, unakaa sana mahotelini, so why unakaa hotelini si uchukue apartment tu? Lakini sio kwamba kusema eti nahamia, hii the way navyoenda tu nahitaji kukaa sehemu ambayo ni permanent,”alisema.

Kuhusu aina ya biashara atakayofanya jijini Nairobi AY alisema,
“Unajua hizi biashara zetu, shop, club , pub, yaani vitu ambavyo
vinazunguka mazingira yetu, huwezi kusema yaani hapa hapa nifungue duka
la spea za magari, labda uwe na uzoefu na hiyo side lakini kama huna
uzoefu na vitu kama hivyo ni bora ucheze na vitu ambavyo vinakuzunguka.”