BANANA AKERWA NA MIMBA YA DADA YAKE

Akisemezana na kituo kimoja cha televisheni cha jijini Dar juzikati, Banana alisema kuwa kwa kipindi kile hakutarajia kama mdogo wake angepata ujauzito ndiyo maana baada ya kupata taarifa hiyo alikasirika.

 
MMILIKI wa B-Band, Banana Zorro amefunguka la moyoni kuwa, mimba aliyopata dada’ke, Maunda Zorro mwaka jana ilikuwa ikimkera hivyo akamnunia.

“Kusema ukweli hata yeye baada ya kupata ujauzito hakuweza kuniambia moja kwa moja, akamwambia mke wangu, nilikereka sana lakini nilimsamehe baada ya kupata mtoto,” alisema Banana.