Mnyika,Dk Slaa Na Lema Kuuawa

John Mnyika,Mbunge wa Ubungo
 CHADEMA kimetoa taarifa kuwa viongozi wake wakuu hapo juu,wanataka kuuawa na usalama wa taifa.Kimesema kuwa wanazo habari za uhakika na wahusika watatajwa mahakamani itakapobidi.kimesema kama usalama wa taifa wana mashaka na madai yao,basi waende mahakamani.

Dk.Slaa akisalimiana na wananchi Walipokuwa kusini majuzi
Dk.Slaa wakati wa Mkutano wa Movement For Change M4C viwanja vya jangwani
Godbless Lema aliyekuwa mbunge wa Arusha na mjumbe wa kamati kuu CHADEMA.
Pia CHADEMA kimekanusha kuhusika wala kuunga mkono mgomo wa madaktari,hakijawahi kushawishi,kufanya vikao nao kwa nia hiyo.Bali CHADEMA inatetea haki za watanzania wote wanaonyanyasika madaktari wakiwemo.
CHANZO
TAARIFA YA HABARI CHANEL TEN SAA 1 JIONI