"NAWAPENDA WANAUME WA KIZENJI KWA SABABU WANAJUA KUPENDA"......BABY J
MSANII wa ngoma ya ‘Bwashee’, Baby J,
amedai kuwa wanaume wengi wa Tanzania Bara si wapendaji bali wengi ni
wale wanaotaka kumchezea mwanamke na mwisho wa siku wanamtema tofauti na
wanaume wa Visiwani ambao hupenda na huwa na mapenzi ya dhati kwa
mwanamke.Mwandishi wetu alifanya
mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya muziki wake pamoja na maisha
kwa ujumla ndipo alipoitoa ishu hiyo, kwa madai kuwa wenaume wengi Bara
wanapenda kutoka na mwanamke mrembo mwenye kila aina ya mvuto na ndiyo
maana wanakuwa na tabia ya kuacha acha hovyo.
Alidai kuwa Zanzibar wanawake wengi ni wale ambao wanaovaa baibui muda
wote na hawana tabia ya kuonyesha miili yao na ndiyo maana unakuta hata
wanaume hawana tamaa ya kutamani kila mwanamke wanayemuona mbele yao.
“Hakuna wahalibifu kama wanaume wa Dar yani ukicheka tu
umekwisha, unajua hii ni tofauti sana na wanaume wa Visiwani na nahisi
inatokana na wadada wenyewe kuvaa nguo za mitengo mno ambazo huacha
sehemu kubwa za mwili zikiwa wazi hivyo humfanya mtoto wa kiume atumie
kila njia kukupata,” alidai.