WAGANGA WA KIENYEJI WAMFILISI AISHA MADINDA


MKATANYONGA ‘mstaafu’ wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ Aisha Mbegu ‘Aisha Madinda’ amedai kupukutishwa fedha na waganga wa kienyeji kwa kile anachotaja kuwa ni kujitibu ugonjwa sugu wa miguu.Mnenguaji huyo aliiambia Mpekuzi hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuwa, ‘tiba za Kiswahili’ zilimfilisi na kumwacha fukara kama si rofa na kwamba sasa ameanza kujipanga kurudisha hadhi yake iliyotoweka kutokana na mikasa ya kimasha.
 “Yaani baada ya kuombewa sasa hivi mambo yangu ni tambarare, naenda kanisani na ninayafurahia maisha haya kwa kweli maana nilihangaika sana kwa waganga, nimepoteza mali nyingi, lakini kwa maombi nimepona bila gharama,” alisema Aisha.


Mkatanyonga huyo amekuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na maumivu ya miguu yaliyomfanya aupe kisogo muziki wa kidunia na kukimbilia kanisani kuombewa, jambo ambalo wadau wamesema huwenda likamsaidia kukwepa skendo za ngono na matumizi ya dawa za kulevya ambazo amekuwa akihusishwa nazo.


Mwaka  2010  msanii  huyu  aliandamwa  na  skendo  ya madawa  ya kulevya na picha  chafu za utupu.......

HONGERA  SANA KWA  KUACHANA NA  WAGANGA  NA  KUMRUDIA  MUNGU....NAAMINI  VITUKO VYOTE  VITAKOMA