Mashindano Ya Kusaka Vipaji Ya Kabati Katiba Star Search Iringa Yafikia Patamu


 Majaji  wa  shindano  ya Kabati katiba star search wakiwa katika  picha ya pamoja na mdhamini mkuu  wa mashindano hayo mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wa  pili  kushoto ,wengine ni Agnes Muba Temy Mahondo na jaji mkuu Edo Bashir ( wa  pili kulia) na jaji mwingine  ni Dj Yeyo hayupo  pichani
 Mmoja kati ya  washiriki  akionyesha  uwezo  wake katika  shindano hilo la kabati katiba Search  ambalo lipo kwa ajili ya  kuibua vipaji vya  wasanii mkoani Iringa
Hawa  ndio  walioingia katika  kinyang'anyiro cha kuwasaka  wasanii wasanii 10 kati ya 25 waliopita awamu ya kwanza

Shindano la  kuwasaka  wasanii  wasanii  bora 10 kati ya 25  walioingia katika mchuano wa  kusaka tuzo maalum ya mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kupitia  shindano lake alililibuni na kulipa  jina la kabati katiba  Star Serach limefanyika leo katika ukumbi  wa Twistars mjini Iringa.

Akizungumza na mtandao       wa  www.francisgodwin.blogspot.com ,mratibu  mkuu  wa shindano  hilo Rashid Msigwa amesema kuwa  tayari  wasanii 10  wamepatikana kwa ajili ya  kuingia hatua ya fainali katika  shindano hilo ambalo amedai kuwa  limekuwa na mvuto  zaidi .

Msigwa amesema  kuwa  awali  wasanii  walikuwa  wakionyesha uoga katika jukwaa ila kwa sasa  wameonyesha  kujiamini  zaidi.

Aliwataja  wasanii  walioingia hatua ya  fainali  leo kuwa ni  Alfred Madembwe,Adimaya Mlawa,Humphrey Sambala,Mohamed  Mpangala, Jackson Mam,Henry Said, Edga Bosco , Emmanuel Mgata , Julius Kimata na Adam Kayombo.

Huku Jaji mkuu  wa shindano hilo Edo Bashir akieleza  kufuruhishwa kwake na jinsi ambavyo  wasanii  hao  wanavyojituma katika  jukwaa na kuwa  upo uwezekano  wa mkoa wa Iringa  kupitia shindano hilo  kutoa  wasanii bora  zaidi ambao  wanaimba vizuri kuliko hata  wasanii  wakubwa hapa nchini.