Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza kuhatarisha ndoa yake.
“Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza: “Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”
Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte, Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume