KAMPUNI YA HONDA YAZINDUA TAWI LAKE MWANZA



Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akizindua tawi jipya la Kampuni ya Quality Motors Limited mkoani Mwanza, kampuni inayo jihusisha na usambazaji na uuzaji wa pikipiki, majenereta, na vifaa mbalimbali vya kampuni ya Honda nchini Tanzania.
Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akijaribu ubora wa moja kati ya mali zilizopo kwenye tawi hilo jipya huku akishuhudiwa na wadau wa karibu wa kampuni hiyo.
Ufunguzi wa tawi hilo utakuwa na manufaa mengi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwani wataondokana na adha ya nishati ya umeme ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika utendaji kazi wao wa kila siku hali inayosababisha kuingia katika gharama za ziada zinazokwamisha maendeleo kutokana na kipato chao duni, ikumbukwe kuwa wakazi wengi hususani wa visiwani hutumia majenereta kama chanzo cha nishati ya umeme kwa viwanda vya usagaji na ukoboaji nafaka, umeme wa majumbani maduka ya kuchaji simu, karakana za uchoeleaji na kadhalika. 
Uzinduzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka ambapo usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ukiendelea kuwa tegemeo kwa wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na tozo nafuu la nauli, hali inayo wafanya wananchi wengi kuufanya usafiri huo kuwa kimbilio lao
Mteja wa kwanza katika duka la Honda Mwanza bw. Vicent Hariah kutoka kampuni ya African Wheels and Tyres LTD akikabidhiwa pikipiki yake mara baada ya kuinunua.
Picha ya kumbukumku... Hadi kufikia mwezi march 2012 halmashauri ya jiji la Mwanza ilikuwa na madereva wa pikipiki za biashara zaidi ya 6,000 wanaotambulika nao wamekuwa wakiongezeka siku baada ya siku.